NILIFIKA MWISHO (LIVE) Lyrics
- Genre:Gospel
- Year of Release:2023
Lyrics
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Uchumi ulizorota nchini mwangu Kenya
Biashara za watu wengi zikaporomoka
Makampuni ya benki nayo katufuata hima
Ili wakanadi mali walipie madeni
Nikauliza Yesu wangu yapi haya yanatendeka
Kaniambia umefika mwisho naja nikusaidie
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Walo kuwa marafiki tulo kula nao
Wakageuka hasidi maadui wakubwa
Sikujua ukifilisika marafiki huwa maadui
Wengi walinishawishi niende kwa waganga
Nikashikilia imani 'kakumbuka Yesu akisema
Yeye atakuwa nami wala hataniacha
Jina langu limeandikwa vigajani vya mikono yake
Hata vita vikichacha Yesu atanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Wimbo huu nimeimba jili yako ndungu dada
Ulofika mwisho wewe ulogonga mwamba
Madeni kulia kushoto yamekuzunguka
Chuki nayo imezidi wala hujitambui
Mwanadamu hugeuka sio kama Yesu
Ndiye rafiki wa kweli kati ya dhoruba
Tega sikio la kiroho usikie sauti yake
Asema umefika mwisho naja nikusaidie
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia
Nilifika mwisho nikagonga mwamba
Lakini Yesu akaja akanisaidia